Kuwa Chuo cha Matibabu, ustawi wa wanafunzi wetu ni wa umuhimu mkubwa. Usimamizi wa Chuo utahakikisha kuwa mazingira ya chuo yanafaa kwa mchakato wa kusoma na kuishi.
Chuo kina kiwanja kipatacho hekari 30 kilichozungushiwa ukuta na zimewekwa kamera za CCTV na walinzi kwa masaa 24.
Mazingira ya Kusomea yanakidhi mahitaji ya baraza la NACTE na baraza la wafamasia .Vyumba vya madarasa ni vya kisasa vyenye vifaa vizuri na vya kutosha kuzuia msongamano.
Mabweni yetu ni ya kisasa yanayojitegemea (bafu na choo ndani).
Usimamizi wa GSMC umejitolea kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapewa mazingira bora ya kujifunza wakati wote.